Tuesday, 23 June 2015

SUGU ASHINDA KESI,AKABIDHIWA MTOTO WAKE.

Sugu na Mwanae Sasha.
Atimaye Mahakama ya mwanzo,Manzese jijini Dar es salaam leo,imempa rasmi Mh,Joseph Desderius Mbilinyi"Sugu"umiliki wa mtoto wake,Sasha.
Hii ni baada ya Mh,Sugu kumshitaki mzazi mwenzie Bi,Faiza Ally kumlea kinyume na maadili mtoto wao huyo,kupitia ushahidi wa picha uliowasilishwa Mahakamani hapo,Mahakama imejiridhisha na kumkabidhi Mh,umiliki wa mtoto wake.........
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Bi,Faiza Ally mama wa mtoto ameonyesha kutoridhishwa na Hukumu hiyo na kuonyesha nia ya kukata rufaa Mahakama ya juu,kudai arejeshewe umiliki wa mtoto wake.........
Faiza & Mwanae Sasha.


SIELEWI JOSEPH AMESHINDAJE KESI- USHAHIDI WA PICHA PEKE YAKE SIONI KAMA UNATOSHA MIMI KUPOKONYWA MTOTO WANGU- MTOTO WANGU NI MDOGO SANA ANANIHITAJI SANA - NA SITA RUDI HATA IKIBIDI KUUZA KILA NILICHO NACHO KWA AJILI YA KUSIMAMIA HILI- SIJAPEWA NAFASI NIMEPELEKWA MAHAKAMANI IJUMAA NA LEO JUMANNE NIMEPEWA HUKUMU/ MWANANGU ACHUKULIWE..... HAPANA ! SITARUDI NYUMA NA HAITAKUA RAHISI NINAKATA RUFAA NA KUTAFUTA WAKILI WA KUNISIMAMIA HILI- MWANANGU ANASOMA VIZURI ANAISHI VIZURI NA NAAMINI KWENYE MIKONO YANGU YUKO SALAMA ZAIDI YA KOKOTE/ YAANI KUHUSU KUKOSA KUKAA NA MWANANGU NI BORA KUFA KULIKO KUISHI NIKIMUONA SASHA ANA LELEWA NA MAMA MWINGINE IKIWA MIMI MAMA YAKE NIKO HAI NA MAKINI KATIKA MALEZI YA MTOTO WANGU- NINA NDOTO NA MWANANGU NYINGI SANA - NAHITAJI KUISHI NAE YEYE NDIO KILA KITU KWENYE MAISHA YANGU/ NAMPENDA SANA MWANANGU NA SIJASHINDWA KUMLEA- NAONA UCHUNGU SANA KUPELEKWA MAHAKAMANI NA KUPOKONYWA MTOTO WANGU BILA SABABU ZA MSINGI . SITAOGOPA CHEO CHAKE CHA UBUNGE KAMWE- NITASIMAMA KAMA MAMA MWENYE HAKI KWA MTOTO WAKE ...😭😭😭MUNGU NAOMBA NIELEKEZE.NISIMAMIE NA UNIHUKUMIE HUU UKATILI NINAO FANYIWA NA BABA SASHA .....Alimaliza"Faiza Ally"..


No comments: