Wasanii wawili wakongwe wa hip hop nchini Afande Sele na Mr,II{Sugu}wameingia kwenye headline baada ya wawili hao kuanza kunangana ambapo Afande Sele ameonyesha kumshutumu Sugu akidai amekuwa Bungeni kwa maslahi yake na wala si kuwatetea wasanii.
Akisisitiza hilo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EA RADIO,Afande amesisitiza kwa kudai Mr,II amekuwa msaliti hata katika harakati alizozianza{Antivirus}kwa kuwaacha njia panda wasanii wenzie waliojitolea kuungana naye katika harakati hizo na kusababisha wasanii hao kurudi nyuma,wakiishia kuomba msamaha kwa aliyekuwa mpinzani wao mkubwa{Clouds Media group},
Afande amedai imefika wakati sasa kwake na Wasanii wengine walioliona hilo kupambana kuingia Bungeni kutetea maslahi ya Wasanii na kazi zao
Akizijibu tuhuma hizo Sugu amedai,Afande amekurupuka na hoja yake,ambayo amedai haikuja wakati husika na pia iliyojaa chuki,akisisitiza kuwa hata wana Mbeya Mjini waliomchagua kuwaongoza KWA MUHULA UNAOISHIA watashangaa kusikia eti yeye yuko Bungeni kwa maslahi ya wasanii na wala si wao waliomchagua,
Akifafanua hilo Sugu amedai japo kauli ya Afande si sahihi pia anatakiwa afahamu kuwa kuwatetea wasanii ama kutowatetea ni matakwa binafsi na wala halimlengi sana kwa kuwa yeye yuko Bungeni kwa niaba ya wana Mbeya mjini.
Source-EA RADIO & EATV.

No comments:
Post a Comment