Monday, 13 July 2015

Majambazi warushiana risasi na Polisi, Clock Tower jijini Dar

Majambazi wakiwa chini ya mikono ya Polisi.
Majambazi sita wametiwa nguvuni na Polisi katikati ya jiji la Dar es salaam,baada ya Majambazi hao  kurushiana risasi na polisi,kwa takriban nusu saa na atimaye kukamatwa,

Kama taarifa hii ya ujambazi ilivyoripotiwa awali kuwa Majambazi hawa walikuwa katika jaribio la kutaka kufanya tukio la kijambazi ndani ya Bank ya Exim{Clock Tower Branch}jijini Dar es salaam.
Ila ukweli toka kwa mtoa taarifa hii amethibitisha kuwa Majambazi hao hawakuiba wala kuingia kwenye Bank ya exim ila walikuwa wanafuatiliwa na polisi, kwenye gari aina ya Noah toka mitaa ya posta ndipo walipofika round about ya clock tower nakuanza kurushiana risasi, watatu kati yao wametiwa nguvuni,ambapo waliotiwa nguvuni walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota spacio.
Jambazi likiwa limetaitiwa na Polisi.

moja ya Majambazi akiwa chini ya mikono ya Polisi.

Raia wakiwa wamejaa kushuhudia tukio zima.

No comments: