![]() |
| Mkuu wa Takukuru mkoani Singida Bwana Joshua Msuya |
Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa Takukuru mkoani Singida
Bwana Joshua Msuya amesema Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amekiuka sheria ya
kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 katika zoezi linaloendelea
la kura za maoni ndani ya vyama vya siasa.
Katika hatua nyingine Bwana Msuya amewatahadharisha wagombea wote
wa ngazi mbalimbali watakao jihusisha na kutoa rushwa iwe ya fedha au
vitu,vifaa vya michezo, madawati watakuwa wamekiuka sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11/2007 na sheria ya uchaguzi cap.343 r.e 2002
na pia sheria ya gharama za uchaguzi namba 6/2010.
Katika jimbo la Singida kaskazini wa tia nia saba ambao wanagombea
ubunge kwa tiketi ya CCM, wametishia kujitoa katika kinyang'anyiro hicho
kufuatia msimamizi wa uchaguzi kumwachia mgombea mwenzao ambaye ndiye
mbunge wa jimbo hilo kutokufuata masharati ya sheria za uchaguzi jambo
ambalo limekuwa kero hadi kutumia vijana wa shule kuonyesha vipeperushi
vyake wakati wa mkutano wa kujinadi.
![]() |
| mbunge wa Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, |
ITV haikuishia hapa ilifanya juhudi za kumwona kaimu katibu wa CCM
mkoa wa Singida ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mkoa Bwana Aluu Segamba,
amekiri kuwepo kwa matatizo hayo na kuchukuwa jukumu la kumbadilisha
msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na kumweka mwingine.
Baadhi ya majimbo ya uchaguzi yenye wabunge ambao wameamua kutia
nia ya kugombea tena wamekuwa wakioneka wao ni chanzo kimoja wapo
kikubwa cha kuvunja mashariti ya uchaguzi na kuwasababishia wenzao kuwa
na malalamiko mengi,hadi kufikia hatua ya kuiomba serekali kupeleka
maafisa wa takukuru na polisi kwenye mikutano ya kujinadi kugombea
ubunge.
Chanzo-ITV.


No comments:
Post a Comment