Monday, 27 July 2015

Yaliyojiri Mkutano wa UKAWA na Wahariri, Makao Makuu ya CUF

Ujumbe huu ndio uliotumwa:

Habari za leo ndugu Mhariri, Ukawa watakuwa na Press Conference leo Saa 8:30 alasiri Ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) Buguruni. Wanaomba mwandishi na mpiga picha. Siku njema.

Ieleweke kuwa, Press Conference hii ya saa 8 mchana si ya CUF bali ya UKAWA. Inafanyika Ofisi Kuu ya CUF Buguruni.

Muda huu Lipumba, Mbowe, Mbatia na Makaidi pamoja na viongozi wengine wa vyama hivyo tayari wapo Buguruni kwa ajili hiyo.
===============

Kwa sasa mwenyekiti mwenza, ndugu James Mbatia ndie anaeongea. Ni rai ya UKAWA kwa kila mtanzania ambae yuko tayari kuondoa mfumo kandamizi wa CCM kuungana nasi. Tunachukua fursa hii kumualika waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli kujiunga na UKAWA. Ni mchapakazi makini na mtekelezaji wa majukumu, UKAWA ndio tumaini la Tanzania, tusikubali kunyamaza pale ambapo sauti zetu zinazimwa kwa lazima. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA, 

                                                       UKAWA ndio tumaini letu.

MASWALI

  1. Mnamualika au mnamkaribisha
  2. Vyama vilikuwa vinasema Lowassa ni dhaifu, leo amekua Imara?
  3. Mnamkaribisha kuingia chama gani maana UKAWA ina vayama vingi?
  4. Akikubali kujiunga na nyinyi leo hii mtakubali agombee nafasi ya urais?
  5. Lini mtamtambulisha mgombea wenu urais?



Lipumba: Maswali ya ufisadi katika Tanzania ni maswala ya Mfumo, mfumo wa siasa ndio unaoendeleza ufisadi, Lowassa ameachia madaraka mwaka 2008, katika kipindi hiki ufisadi umeongezeka au Umepungua? Pia yeye mwenyewe alisema mwenye ushahidi aende mahakamani.


Swala la kumtangaza mgombea urais ni utaratibu wa vyama,Lakini nina uhakika Mwanzoni mwa mwezi August tutakuwa tumepata mgombea urais ambae atapeperusha bendera ya UKAWA.

Kuhusu Lowassa kupewa nafasi ya kugombea urais: Hilo ni swala la mchakato, mgombea urais atapatika kwa utaratibu ambao upo kikatiba.

Mzee Makaidi (NLD)
Lowassa ni mtu safi hadi pale atakapobainika mahakamani ni mchafu.

Mbatia
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake. Watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi. Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri.

Mbowe: Mazungumzo yameshafanywa hivyo hawezi kuongea na amesema kuhusu picha za Lowassa kuwa kwenye kikao cha CHADEMA zimetengenezwa.

Lipumba
Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.

No comments: