REVENGE!
Katika kile kinachoonekana kama kejeli kwa mke wake wa zamani aliyekorofishana naye, mtangazaji maarufu Gardner G. Habash, ametundika picha kwenye akaunti yake katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha akiwa amempakata mwanamke mjamzito.
Katika kile kinachoonekana kama kejeli kwa mke wake wa zamani aliyekorofishana naye, mtangazaji maarufu Gardner G. Habash, ametundika picha kwenye akaunti yake katika mtandao wa Instagram ikimuonyesha akiwa amempakata mwanamke mjamzito.
Gardner, mume wa ndoa wa
nyota wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo, anayesadikika kuwa na
matatizo ya uzazi, aliiweka picha hiyo akiificha sura ya mwanamke huyo,
lakini akionyesha kulishika tumbo huku akiachia tabasamu na kusindikizia
na maneno kuwa mambo mazuri yako mbioni kuja.
Katika maoni mbalimbali ya
wadau waliozungumzia suala hilo, baadhi walimpongeza kwa kumpata
mwanadada na kumpa ujauzito, huku wengine wakihoji kama huyo ndiye
shemeji au wifi yao.
Wapo waliokwenda mbali
zaidi na kudai mtangazaji huyo wa zamani wa Times FM, alikuwa amefanya
kitendo hicho makusudi ili aweze kumkejeli Jide, ambaye alikaa naye kwa
muda wa miaka kumi pasipo kupata mtoto.
“Jamani hivyo siyo vizuri
maana anamkejeli tu dada yetu Jide, sijui anaona raha gani kumuumiza
mwenzake moyo,” aliandika mdau mmoja.
Risasi Mchanganyiko
lilimtafuta Gardner na kutaka kufahamu kuhusu ukweli wa picha hiyo na
kama alikuwa na lengo la kumkejeli mwandani wake huyo wa zamani.
“Yaa, ni kweli picha
nimeweka mimi..lakini si kwa lengo la kumkejeli Jide, kwa nini
nimkejeli? Mimi sina matatizo naye mbona, ni picha tu nimeweka..
“Huyo ni shemeji yangu, mke
wa mdogo wangu mmoja kifamilia. Lakini usijali, wiki hii nitamwonyesha
picha nzima ili watu wamtambue na nitawaeleza kwa kirefu,” alisema
Gardner, ambaye pia ni mdau mkubwa wa muziki.
Wawili hao waliingia katika
mtafaruku miezi kadhaa iliyopita na tangu wakati huo, hakuna hata mmoja
kati yao aliyeweza kuzungumzia suala hilo moja kwa moja zaidi ya
mafumbo wanayoyatoa kupitia akaunti zao katika mitandao ya kijamii. Jide
hakupatikana kuzungumzia picha hiyo.

No comments:
Post a Comment