Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeonya kuhusu matumizi ya helikopta
maeneo ya hatari na mikusanyiko ya watu katika kipindi cha uchaguzi.
Chadema imekuwa ikitumia helikopta katika harakati zake za siasa tangu
wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kwenye chaguzi ndogo na
operesheni zake mbalimbali za kisiasa. Mwaka 2010, CCM nayo ilifuata
nyayo za Chadema na kutumia helikopta
kwenye uchaguzi mkuu na ikatumia tena katika mchakato wa kupata mgombea
wake wa urais mwaka huu.
Hata hivyo, mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amesema hatatumia helikopta katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu.
Katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa TCCA, Charles Chacha, ameonya matumizi ya helikopta katika kampeni za uchaguzi kwa maelezo kuwa kuna uwezekano wa kuleta athari za kiusalama. “Mamlaka inatambua kwamba matumizi ya helkopta wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015 yanatarajiwa kuongezeka na kuna uwezekano wa kuleta athari za kiusalama kwa maisha ya watu na mali pamoja na watumiaji wa vyombo hivi. “Pia vitendo vya kuning’iniza vitu kama mabango ya matangazo mbalimbali kwa kutumia ndege (helkopta ikiwamo) yanaweza kuleta hatari endapo sheria na taratibu zinazohusiana na matumizi hayo hazitazingatiwa,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imezungumzia mahitaji ya jumla ya kiuendeshaji, usalama wa eneo la kutua na kuruka, usimamizi wa chombo kikiwa angani na usalama kwa umma, kuchukua na kuangusha vitu ardhini na kupeperusha mabango angani na kutoa taarifa za matukio.
Chanzo-#Mtanzania.

No comments:
Post a Comment