Mjumbe wa shina namba 20 wa mtaa wa
ulongoni a, kata ya gongo lamboto jijini Dar es Salaam, amekamatwa baada
ya kukutwa akiandikisha majina na namba za vitambulisho vya kupigia
kura.
Mjumbe huyo wa CCM anayefaahmika kwa jina la Mustapher Juma
ametiwa nguvuni baada ya kuendesha zoezi la kuandika majina na namba za
vitambulisho vya kupigia kura huku akiwalaghai wenye vitambulisho hivyo
kuwa watakuwa wanufaika wa kwanza pindi taasisi ya fedha ya umoja Saccos
itakapoa anza kufanya kazi zake.
Katika mahojinao yake na ITV mjumbe huyo wa shina namba 20 wa mtaa
wa Ulongoni A, amekiri kupatia fomu maalum ya kuandika majina na namba
za vitambulisho vya kupigia kura huku akisisitiza kuwa alipewa kazi hiyo
na moja ya viongozi wake wa tawi bila kujua matumizi ya namba hizo.
ITV ilipojaribu kumtafuta Bw Thomas Mwita Kimbaru anayedaiwa
kumpatia fomu hiyo mjumbe huyo wa shina, alisema hahusiki na chochote na
kwamba si msemaji wa chama, katika hatua nyingine mtandao wa asasi za
kiraia za kutazama uchaguzi nchini umeonyesha kutokurishwa na vitendo
mbalimabli vilivyoanza kujitokeza katika zoezi la kampeni hasa matumizi
ya lugha za matusi huku wakiitaka tume kuhakikisha inasimamia sheria.
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi kwa sasa maandalizi yote ya
uchaguzi yako vizuri huku ikiendelea kusisitiza vyama kuhakikisha
vinatii na kuheshimu misingi ya siasa safi na kutokuwa chanzo cha
kufanya uchaguzi kutokuwa huru na haki.
Chanzo:-ITV

No comments:
Post a Comment