Wizara ya Afya nchini Kenya imetoa orodha ya peremende zenye bangi.
-Inadaiwa peremende hizo zimesambazwa hadi hapa kwetu Tanzania.
Wizara ya afya nchini Kenya imetoa orodha ya Peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi, huenda zimesambazwa hadi Tanzania.
Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashangaza wazazi, barua ambayo ilitiwa sahihi kwa niaba ya maabara ya Serikali, ilisema kuwa baadhi ya sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu, keki na maandazi zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Licha ya watoto kuzipenda bidhaa hizo, Serikali inataka vipigwe marufuku na kuondolewa kabisa madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kuziuza.
Kupitia kwa barua kwenda kwa wakuu wa afya wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya imewaamrisha Maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu zingine bidhaa hizo zinaweza kupatikana.
Chanzo: BBC

No comments:
Post a Comment