Thursday, 27 August 2015

TAARIFA-UKAWA WARUHUSIWA KUZINDUA KAMPENI JANGWANI JUMAMOSI.

UKAWA kutumia uwanja wa Jangwani jumamosi

Malalamiko ya UKAWA ya kukatazwa kutumia uwanja wa Jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na Tume ya Taifa ya uchaguzi na taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene imesema kuwa hafla hiyo itafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
Mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene


Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa serikali kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa malalamiko yao. 
NB:-HII HAPA NI BARUA TOKA KWA MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI-NEC...
 

Uzinduzi wa Kampeni za UKAWA - Jangwani
TUMEUPATA UWANJA. Tukutane Jumamosi hii 29.08.2015 pale viwanja vya Jangwani. Tafadhali SHARE na wengine.
Posted by Team Lowassa on Wednesday, August 26, 2015

No comments: