![]() |
| Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA , James Mbatia |
Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala- Dar es Salaam wamemzuia Mgombea wa
UKAWA, Edward Lowassa kuzindua kampeni
zake kwenye viwanja vya Jangwani Jumamosi
ya 29 Agosti , 2015 .
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA , James Mbatia
amesema jiji umewagomea kufanya uzinduzi
huo Jangwani kwa madai kuwa tayari kuna mtu
mwingine ambaye ameshalipia uwanja huo.
Mbatia anasema pamoja na kufanya juhudi za
kuomba kutajiwa aliyelipia uwanja huo ili
wazungumze naye , Jiji walikataa.
Mbatia anasema viongozi wengine wa UKAWA
wanashughulikia suala hilo ikiwa pamoja na
kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
Damian Lubuva kuingilia kati.
NB:-VIDEO Mh,JAMES MBATIA AKIONGEA NA WANAHABARI KUHUSIANA NA HILO.
Chanzo-Clouds Media


No comments:
Post a Comment