Monday, 14 September 2015

KEBEHI ZA ORIJINO KOMEDI KWA MGOMBEA URAIS{UKAWA}ZACHUKUA SURA MPYA.

Naanza kwa kusema kuwa ieleweke kwa mwanadamu mwenye hekima,suala la Afya huwa ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu.
Katika Harakati hizi za kampeni .tumekuwa tukijionea jinsi kundi la Orijino Komedi likishiriki kampeni za CCM kwa kumkashifu mgombea urais kupitia Ukawa,huku wakisahau yaliyomkuta mshiriki mwenzao Vengu ambaye mpaka sasa anajiuguza kitandani kutokana na Laana ya kumuigiza Mh,Augustino Lyatonga Mrema kidizaini,tufahamu ya kwamba kwa namna moja Fimbo ya Mungu haina mipaka ya kuhukumu,unaweza kuhukumiwa hapa hapa duniani,kama ilivyokuwa kwa mwenzao huyo,anayeugulia kitandani na huku aliyekuwa akimkebehi kwa maradhi yu bado anadunda na Maisha yanaendelea......
Tuelewe njaa zetu zisitufanye tukosane na Mungu kwa kujiingiza kwenye Laana za kujitakia....

No comments: