Rapa wa nchini Kenya, CMB Prezzo amezikonga nyoyo za wengi baada ya
kuasili mtoto wa kiume kutoka kituo cha watoto cha Grace Community
Children’s Home na kumtambulisha kwa dunia kama mwanaye ambaye
anatambulika sasa kama Gabriel Prezzo.
Prezzo
ametaka mashabiki wake kutambua kuwa mwanae huyo ni mwanachama mpya wa
kundi lake la CMB, hatua ambayo imempatia pongezi nyingi kutoka kwa
wapenzi wa sanaa yake, akiwa tayari anafahamika kuwa ni baba wa mtoto
mmoja wa kike.
Hatua hii ya Prezzo inakuwa ni sawa na ile ya msanii wa muziki Bahati kutoka nchini Kenya, ambaye naye aliasili mtoto mwishoni mwa mwaka jana.
Hatua hii ya Prezzo inakuwa ni sawa na ile ya msanii wa muziki Bahati kutoka nchini Kenya, ambaye naye aliasili mtoto mwishoni mwa mwaka jana.
![]() |
| staa wa muziki wa nchini Kenya Prezzo akiwa na mtoto aliyemuasili na kumbatiza jina Gabriel Prezzo |

No comments:
Post a Comment