![]() |
=========
Anaeongea kwa sasa ni Tundu Lissu na anaongelea utaratibu wa kukabidhi madaraka endapo watashinda kwa chama pinzani.
Mnyika: Anaongelea kauli ya NEC kuhusu kusema CHADEMA wanawapa tabu na anasema NEC ni shida. Anataka NEC waeleze ni lini wataalamu wa TEHAMA watakagua mfumo mzima. Anasema sasa hivi daftari limekuwa siri, anataka wataalamu wakakagua database ya tume, Lubuva anasema ni mara ya kwanza kusikia hili ombi wakati walilitoa Mbeya.
Mdee: Anasema kuna mchezo mchafu unachezwa na tume, anataka kutolewa ultimatum kwa kuweka majina daftari la uandikishaji, watu hawana hakika kama majina yao yatakuwepo na wasiadahike na kauli ya tume kwamba kila mwenye kitambulisho atapiga kura. Asante sana.
Anaeongea kwa sasa ni Taslima na anatoa nukuu za mwalimu Nyerere kuhusu uongozi wa Tanzania.
Mama Regina: Niwakumbushe jambo moja tu, kura yako ni haki yako, kura yako ni hatma yako, niombe kura kwa ajili ya mume wangu Edward Lowassa. Asanteni sana.
Mbatia: Watanzania wameshakubali Rais wao ni Edward Lowassa, Tanzania bila CCM inawezekana, Rais Kikwete ajiandae kisaikolojia kukabidhi madaraka. Wanajaribu kumchafua Lowassa. Kwenye makarasi ya kupigia kura hamna UKAWA, chondechonde msiharibu kura na jina la Edward Lowassa ni la nne. Wanasema mimi ni mshirikina, ni kampeni chafu za CCM na wanajua CCM walioliongoza taifa hili kwa nguvu za giza kwa miaka 24.
Sumaye: Watanzania wameamua mabadiliko ni lazima mwaka huu, walituahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Haiwezekani Rais kutumia nusu ya muda wake wa madarakani akiwa nje ya nchi, Lowassa akiingia madarakani itabidi alipe zaidi ya bilioni 900 kama faini ya kuwaweka makontracta mabarabarani bila hela. Magufuli alitaka kuvunja TANESCO wakamshika shati, alivunja nyumba ya Tanroads na leo inajengwa palepale. Kwenye urais nani atamshika shati Rais, CCM hata kama ingemleta nani haifai tena kuongoza nchi hii.
Mbowe: Naomba kuwaambia watanzania wenzangu tarehe 24 sio siku ya kulala, itakuwa siku mkesha ya ukombozi wa nchi yetu. Siku ya tarehe 25. Sheria inasema hairuhusiwi kukaa ndani ya mita mia, hesabu mita mia piga kambi. Tunajua haki na tunajua kuilinda haki.
Lowassa: Katika hotuba yangu ilikuwa nizungumze juu ya wanajeshi ila nimesikia ndege imeanguka, naomba tusimame kwa dakika tatu. Kama alivyosema mke wangu, nimekuja kuwaomba kura, mwambie jirani yako naomba kura, zinatakiwa kura nyingi sana karibu milioni 24, kama mzee nyumbani mwambie naomba kura, kama una mshikaji mwambie naomba kura.
Nimemsikiliza Mdee, Mnyika na Mbatia juu ya katiba, lakini mimi nawashauri niachieni nawaahidi nitalifanyia kazi. Pili kwa nini nagombea Urais, nagombea kwa sababu najua nina uwezo wa kugombania Urais, ya tatu ni kwa sababu nimeochoka umasikini, sick and tired. Sitaki kusikia habari ya mlo mmoja kwa siku, narudia umasikini sio amri ya Mungu. Jambo la kwanza naanza na elimu bure na bora, sitaki kusikia mchango wa chaki wala penseli mashuleni.
Kuna watu wananikebehi wananiuliza utaweza, nawaambia nitaweza. Blair alipoulizwa alisema edecution, education, education. Watoto wetu hawawezi kukidhi mahitaji ya soko la dunia, ni very poor quality. Agenda ya pili ni bodaboda na mama ntilie, nitakula sahani moja na bodaboda na machinga.
Vipaumbele vyangu ndani ya siku 100 ni Huduma za uzazi, Nitapunguza foleni Dar, mfumo bora wa kodi. Ikulu hatuendi kwa kelele, tunaenda kwa kura.
No comments:
Post a Comment