![]() |
Mgombea ubunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amezungumzia ajali mbaya ya gari aliyoipata jana usiku alipokuwa njiani akitokea Dar es Salaam kuelekea Lindi.
Nape ameeleza kuwa yuko salama na alipata majeraha madogo ingawa ajali hiyo ilikuwa mbaya kwa kuwa gari lake lilipinduka na kugeuka mara kadhaa baada ya tairi ya mbele ya gari lake aina ya Land Cruiser alilokuwa anaendesha kupasuka.
![]() |
Gari alilopata nalo ajali, Nape Nnauye |
Mgombea huyo wa ubunge alikuwa peke yake kwenye gari hilo na ameeleza kuwa mkanda na ‘air bag’ zilimsaidia kupunguza makali ya ajali hiyo.
“Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia,” alisema.
No comments:
Post a Comment