![]() |
Mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, |
Mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, jana alihitimisha kampeni zake mkoani TANGA huku akiwatahadharisha vigogo wa Jeshi la Polisi kuwa waache ubabe kwa wananchi na kuzingatia sheria za nchi kwani wakiendeleza uonevu atawashtaki kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Mwezi uliopita, Lowassa aliahirisha kufanya kampeni kwenye viwanja vya Tangamano kutokana na watu kuwa wengi kuliko uwezo wa eneo hilo ambalo lilizidiwa na watu kadhaa waliojitokeza kuzimia kwa joto na kukosa hewa.
Akizungumza katika moja ya kampeni zake kwenye viwanja vya Indian Ocean jana, Lowassa alisema baadhi ya polisi siyo waungwana kwani hutumia mabomu na nguvu kubwa kuwashambulia wananchi.
“Napenda kuwatahadharisha tena… nisije nikawashtaki ICC kwa kufanya vurugu na kuwapiga wananchi bila kosa. Waacheni wafanye shughuli zao,” alisema.
No comments:
Post a Comment