Thursday, 29 October 2015

MANENO YA PROFESOR JAY BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI WA KURA ZA UBUNGE JIMBO LA MIKUMI.

Bw,Joseph Haule{Prof,Jay}
Professor Jay
1 hr ·
Naanza Kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma kwa kuniwezesha kufika mahali hapa nikiwa mzima na mwenye afya njema na kunipigania katika kila vikwazo na changamoto mbalimbali nilizopitia, Pili napenda kuwashukuru sana wananchi wote wa jimbo la langu MIKUMI kwa kuniamini, Kunichagua na kunipa Heshima hii ya kipekee na dhamana hii ya kuwatumikia, Nawaahidi nitashirikiana nanyi kwa unyenyekevu mkubwa, kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote bila kujali itikadi za vyama vyetu, Maana Lengo letu kuu ni kuleta mabadiliko na maendeleo ili tuweze kuijenga MIKUMI tunayoitaka, Mwisho kabisa napenda kuwashukuru sana Ndugu, Jamaa na Marafiki zangu wote kwa kuonyesha Upendo na ushirikiano wa nguvu kwa namna moja ama nyingine mpaka kunifikisha hapa nilipo sasa...
MIKUMI MPYA KWA MAENDELEO YA WATU WOTE! Mungu awabariki sana, ASANTENI SANA!!!!
Mp JOSEPH HAULE....

No comments: