Thursday, 22 October 2015

MGOMBEA URAIS KWA TIKET YA CHAMA CHA ADC ATISHIA KUGOMEA MATOKEO UCHAGUZI MKUU 2015

Mgombea Urais kupitia chama cha ADC, Chief Lutasola Yemba

Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kufikia uchaguzi mkuu nchini, Mgombea Urais kupitia chama cha ADC, Chief Lutasola Yemba ametishia kutokukubaliana na matokeo endapo kama uchaguzi ukifanyika pasipo kufuata misingi ya haki na uwazi.
 Chief Lutasola amesema hayo wakati akiongea na timesfm, ambapo ameitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuwa makini kuelekea mchakato huo bila ya kupendelea chama ama mgombea yeyote.
Pia mgombea huyo amewataka wagombea wenzake na viogozi wa vyama siasa kuhamasisha wananchi wajitokeze kupiga kura.
Akizungumzia dhana ya kulinda kura, Chief Lutasola Yemba amesema ili kuondoa sintofahamu ya kukaa ama kutokaa umbali wa mita 200, vyama vya siasa vinatakiwa kuwa na wakala wenye uaminifu wasiokubali kurubuniwa.
Chanzo-Times Fm

No comments: