Wednesday, 28 October 2015

NI FAINALI YA MATOKEO UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR LEO.

Zanzibar.
Waingereza wana msemo maarufu unasema "When the hunted knows how to hunt, (that means) the hunting game is over" Kwa maana "Muwindwaji atakapojua jinsi ya kuwinda, (hiyo inamaana) mchezo wa kuwindana unakua umekwisha !
Alhamdulillah Zanzibar ndio kumepambazuka na leo ni siku ya 3 na siku ya mwisho kwa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar kutangaza matokeo, katika hali isiyo ya kawaida popote Duniani, Zanzibar yenye wapiga kura 503, 836 tu na sio wote ambao wamepiga kura, mpaka sasa Tume ya Uchaguzi bado haijakamilisha zoezi la kumtangaza Rais wa Zanzibar.
Wameahidi kuanza matangazo hayo saa 4 asubuhi ya leo, basi tuzidi kuomba kheri na salama na haki itendeke ili hali ya Zanzibar irejee kama kawaida. Kwani toka kuanza mchakato huu Mji huu umekua shwari sana zaidi utapishana na Askari wa kutuliza ghasia. Japo Wananchi walio wengi wamekua Wastaarabu na kusubiri matokeo rasmi yatangazwe.
Wengine stocks zao zimeshamalizika, wengine wagonjwa wanashindwa kutoka, wengine wanapata sulubu bila hatia, wengine hawajafungua Biashara au kwenda Vibaruani mwao na pesa zimewaishia, wengine hawana pakwenda isipokua Zanzibar, wengine ni Wacha - Mungu na wanateseka, wengine wamekufa hata mazikoni kufika ni shida, kuna watoto wadogo na wazee watu wazima, vilevile wasiojiweza kwa viungo na wasioona pia.
Ewe Mola wetu hakuna aliye juu zaidi yako nawe ndio Mjuzi zaidi na Mfalme wa Milele, kwa Unyenyekevu wote tunakuomba kheri na salama na haki itendeke kwa hakika wewe hupuuzii bali Unapuruzia "...Qad tabayyanar - rush minal ghayyi..." Indeed the Truth is OPEN from lies !
Mola wetu jaalia salama kwa Zanzibar na watu wake na Tanganyika yote.
Mola wetu watie nyoyo za imani Viongozi wetu na haki iwekwe mahala pake.
Mola wetu hakika sisi ni Wadhaifu juu yako, tunaomba tusamehe na tuondoe chuki baina yetu kwa Maslahi yetu sote na kizazi kijacho.
Mola wetu kwa kila mwenye nia mbaya basi ipeperushe nia yake hiyo, na badala yake Upendo ndio utawale kwake.
Mola wetu tunakuomba tuepushe na Dhuluma na zahma...Amin, Amin, Amin !
Niwatakie kila la kheri katika hatma ya Zanzibar na Tanzania nzima...Tuzidi kuomba salama vile ukweli unajulikana.

By @Ally Almafadhy

No comments: