![]() |
Rev,Christopher Mtikila. |
TAARIFA:_
Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Kamanda Jafari amesema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Rev.Mtikila amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze. Akiwa ndani ya gari lililokuwa limempakia lililokuwa linatokea Morogoro na kwamba katika gari hilo walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya. Ambapo Majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Serikali Tumbi-Kibaha.
![]() |
Gari lililokuwa limembeba Rev,Christopher Mtikila baada ya Ajali. |
No comments:
Post a Comment