Thursday, 22 October 2015

UFAFANUZI ZAIDI JUU YA UKOMO WA BARAZA LA MAWAZIRI.


Kwa wale walioomba ufafanuzi kuhusiana na baraza la mawaziri.. Kutokana na katiba ya Tanzania inayotumika ya mwaka (1977) Ibara ya 52- (2) madaraka ya Waziri/Naibu yatakoma pale tu

A:. Endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki dunia

B:. Ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge

C: Ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;

D:. Kama atachaguliwa kuwa spika

E:. Iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;

F: ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo

G: Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 

No comments: