Friday, 30 October 2015

USHAURI WA RICK ROSS KWA MEEK MILL KUHUSIANA NA BIFU YAKE NA DRAKE.


Rapper Rick Ross anajiandaa kuachia album yake ya Black Market, na rapper wake wa MMG Meek Mill ana album inayofanya vizuri sokoni ya Dreams worth more than money.
Wakati Meek anatoa album yake, aliingia kwenye bifu nzito na rapper wa Young Money Drake baada ya kumshutumu kuwa anaandikiwa mashairi yake.
Sasa Rick Ross amepiga story na MTV, akafungukia bifu hiyo na kumpa ushauri mkali wake Meek Mill. “Afanye anachokifanya kufika mbali zaidi, afanye anachojisikia kufanya ili kuifikisha mbali game yake, kuna watu hawanielewi mi niko fair sana na watu wangu” alisema Rick Ross

No comments: