![]() |
| Seleman Abdallah Msindi maarufu kama Afande Sele, |
![]() |
| Hellen B Massawe |
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni msanii
mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya, amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo
Chamwino akidaiwa kutomlipa mjasiriamali Hellen B Massawe kiasi cha
shilingi 1,390,000.
Hellen ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam,
aliliambia gazeti hili akiwa nje ya ofisi za chama hicho mjini Morogoro
kuwa alikopa benki na kufanya kazi ya kutengeneza fulana hizo kwa
wanasiasa wa vyama vingi, lakini ni Afande Sele pekee ambaye hakumlipa
na kila alipomfuata alimtaka kufuata fedha hizo kwa kiongozi mkuu wa
chama, Zitto Kabwe.
![]() |
| Afande Sele |
“Baada ya kuzunguka huku na kule bila mafanikio, hasa baada ya kuambiwa
kuwa chama kisingeweza kumpa fedha kwa vile mgombea huyo alishapewa
ruzuku, aliamua kwenda mahakamani kufuatia ushauri wa polisi kuwa hiyo
ni kesi ya madai. Nimeenda mahakamani na nikapewa samansi ambayo Afande
Sele ameisaini,” alisema.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, Aziz Abood
alishinda Ubunge Jimbo la Morogoro mjini kupitia CCM huku mgombea wa
Chadema, Marcossy Albani akishika nafasi ya pili na Afande Sele
aliambulia nafasi ya tatu.
Chanzo-GPL



No comments:
Post a Comment