KIPINDUPINDU NCHINI.
Jumla ya wagonjwa 106 wamefariki dunia kote nchini kwa kipindupindu hadi kufikia jana kati ya watu 7,598 waliougua maradhi hayo.
Katika Jiji la Dar es Salaam pekee idadi ya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo hadi kufikia jana ilikuwa ni 53.
Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi, aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu hali ya kipindupindu nchini.
Dk. Kitambi alisema hadi sasa mikoa 17 na wilaya 39 za nchi nzima, imeathirika na ugonjwa huo.
Hata hivyo, alisema serikali imefanya jitihada za kupambana na ugonjwa huo kwa kutoa elimu kwa wananchi na kwamba mpaka sasa imetoa Sh. milioni 900 kupambana na maradhi hayo.
“Siyo milipuko yote inakuwa dharura, inakuwa dharura pindi inapotokea madhara, kipindupindu kwa sasa ni tatizo kubwa, kuna magonjwa kama homa ya bonde la ufa, dengue, mafua ya ndege, ifluenza, chikungunya ambayo yaliwahi kutokea na kuleta madhara duniani na nchini,” alisema Dk. Kitambi.

No comments:
Post a Comment