![]() |
| Kanye West |
Kanye West ni moja kati ya marapper wa kimarekani wenye matukio kadhaa kila siku, mengine yamekuwa yakishangaza wazi wazi.
Pengine hili nalo linaweza kukuacha mdomo wazi, na kugundua kuwa Yeezus ni moja kati ya wasanii wanaothamini sana usafi wa Nywele zao. Sasa baba yake Rihanna bwana Ronald Fenty, ambaye amekuwa akisafiri na familia ya Kanye kwenye ‘tour’ tofauti tofauti tangu mwaka 2010, ameliambia jarida la Heat kuwa rapper huyo amekuwa akitumia dola za Kimarekani 500 kwa ajili ya ‘kunyoa’ pekee.
Kama taarifa hii inaukweli, basi kinyozi wake aitwae Ibn Jasper atakuwa anavuna kiasi cha dola za kimarekani 182 500 kwa mwaka kutoka kwa bosi wake Kanye West.

No comments:
Post a Comment