Friday, 27 November 2015

Kashfa Bandarini Dar: Rais Magufuli amsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade.

Aliyekuwa Kamishna wa TRA Rished Bade
Imefika punde, Rais John Magufuli amemtimua kazi Mkurugenzi wa TRA kutokana na kashfa ya bandari iliyopelekea maofisa kadhaa kukamatwa huko.

My take: Tuache muda uongee kasi ya JPJ

Phillip Mpango aliyekaimishwa Ukamishina mkuu wa TRA.
 RAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU TRA

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano - Ikulu imesema kuwa alasiri ya leo, Rais Dk. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Rished Bade.

Rais amemteua Kamishna Phillip Mpango kukaimu nafasi hiyo; na amemtaka Rished Bade kumpa ushirikiano Mpango hasa katika kutafuta ukweli kuhusu makontena 349 yenye thamani ya shilingi bilioni 80/= yaliyotoweka bandarini pasipo TRA kuwa na kumbukumbu zozote za makontena hayo.

No comments: