Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekabidhiwa rasmi ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Baada ya makabidhiano hayo Mhe. Samia, alikaribishwa na watumishi wa ofisi yake ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii kulingana na kauli mbiu ya
‘Hapa ni Kazi tu’.
“Kila mmoja afanye kazi kwa bidii mahala pake pa kazi. Wale ambao kauli mbiu ya Hapa ni Kazi tu, itawapita wakae pembeni… watatusamehe”, alisema Makamu wa Rais
Aidha Mhe. Samia alisisitiza suala la kuendelea kupendana na kushirikiana miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ili kufanikisha azma ya kuleta matarajio ya maendeleo ya Watanzania wanayotaka kuyaona katika uongozi wa awamu ya tano.
Baada ya kutoa nasaha hizo alifanya kikao na Menenjimenti ya ofisi ambapo alitoa uelekeo wa utendaji kazi katika ofisi hiyo hususan kuzingatia kusimamia masuala ya muungano na mazingira ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Aliitaka Menejimenti hiyo kujipanga upya na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwa upande wa masuala ya muungano na mazingira.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
9/11/2015
=====================================================================
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi
yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 9, 2015. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa
mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Nov 9, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais
Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, ….baada ya
makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov
9,2015. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya
Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu
jijini Dar es Salaam, leo Nov 9, 2015. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akipokea zawadi ya Maua kama ishara ya makaribisho, kutoka kwa
mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, wakati
alipowasili kwa mara ya kwanza kwenye Ofisi yake na kupokelewa na
wafanyakazi wake leo, Nov 9, 2015. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan,akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Sazi Salula,wakati
alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa
ofisi rasmi leo, Nov 9,2015. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Eng. Angelina
Madete. |
 |
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi
Binafsi ya Makamu wa Rais, wakati akiondoka baada ya makabidhiano ya
Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 9, 2015 |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati
alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya
kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal.
Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na
vigeregre wakati akiwasili. |

.
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati
alipowasili kwenye Ofisi hiyo leo Nov 9, 2015 baada ya makabidhiano.
Akizungumza na wafanyakazi hao Mama Samia, aliwataka watumishi hao
kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa bidii ili kutimiza Kaulimbiu ya
Mhe.Rais ya ‘HAPA KAZI TU’. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara
zilizo chini ya Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira na Muungano)
alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza leo Nov 9, 2015. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu
Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wanamama
wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara
ya kwanza leo Nov 9, 2015 kwa makabidhiano ya Ofisi na Makamu wa Rais
Mstaafu. |
No comments:
Post a Comment