Friday, 6 November 2015

MAMA LOWASSA AUKATAA UBUNGE VITI MAALUM-CHADEMA.

Mana Regina Lowassa,

Mke wa Lowassa autosa ubunge wa Viti Maalum CHADEMA 

Mana Regina Lowassa, ameikataa nafasi ya ubunge wa viti maalum aliyopewa na kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani. Kwa mujibu taarifa wa kutoka familia ya Lowassa, Regina anaichukulia kwa heshima kubwa nafasi hiyo, lakini anaamini ataweza kushughulikia matatizo ya akina mama na watoto akiwa nje ya Bunge. "Naishukuru kamati Kuu ya chama changu kwa heshima hii kubwa waliyonipa na ninaithamini sana, lakini naamini nitaendeleza mapambano ya kuwaletea akina mabadiliko kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge," amesisitiza mke huyo wa waziri mkuu wa zamani katika taarifa hiyo.
Kamati Kuu ya CHADEMA ilifikia uamuzi wa kumpa Regina nafasi ubunge viti maalum kutokana na mchango mkubwa alioutoa wakati wa kampeni ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia upatikanaji wa majimbo mengi tofauti na uchaguzi wa mwaka 2010.
Chanzo: Mwananchi

No comments: