Sunday, 15 November 2015

NASH MC AENDA AFRICA KUSINI KWA ZIARA YA KUJITANGAZA.

Rapper mkali wa muziki wa Hip Hop Bongo Maalim Nash @maalimnash , yupo nchini Africa kusini kwa ajili ya ziara ya kuongeza wigo wa mziki wake.
Taarifa kubwa ni kwamba rapper Huyo, amekutana na producer mkubwa na mwalimu wa kutengeneza beats za Hip Hop aitwae 9th Wonder.
Kwa mujibu wa ukurasa wake wa Instagram Nash ameandika kuwa alifanikiwa kumpatia baadhi ya Ngoma zake.
Leo Hit maker huyo wa Naandika, atapiga show mjini Johannesburg Hillbrow nchini humo. Je huu ndio mwanzo wake kimataifa??

NI KWA NEEMA TU! Nazidi kumshukuru Mungu kwa kuibariki Safari yangu ya Hapa Jozi na imekuwa ya mambo mazuri Tangu nilipofika,Leo katika Safari yangu ya muziki nimeongeza historia muhimu na kubwa sana kwangu baada ya kukutana na Mpiga midundo Mkubwa duniani wa Hip Hop na pia ni mwalimu wa ufundishaji wa kupiga midundo mtu mzima 9th Wonder na nikapata nafasi ya kumpa Cd zangu Kama unavyoziona,na Jambo la pili kubwa pia nikaonana na mmoja Kati ya vichwa hatari katika Hip hop kwa sasa mzazi Skyzoo,pia nilimpa Cd zangu,nikamwambia kuwa hiyo ni Swahili Rap,akasema if it's Swahili,it's dope,nimekuwa mwenyewe furaha sana siku ya Leo na Tangu nimefikia Hapa. Hili tukio lilikuwa pale Museum Africa (New Town, JHB) baada ya mkutano uliokuwa umeandaliwa na wahusika,yani Jamla squad nusu na robo ilikuwepo. Kuthubutu

A photo posted by Nash Mc (@maalimnash) on

No comments: