Monday, 16 November 2015

Nyumba za wakazi wa Kurasini Shimo la udongo Jijini Dar Zabomolewa.

Wananchi wa Kurasini wamekumbwa na bomoabomoa mda huu na inaonekana hawakupewa mda wa kujiandaa.

Kwa sasa wapo nje na vitu vyao huku tingatinga ikiendelea kubomoa je huu ni uungwana?.

Inadaiwa zinabomolewa kupisha muwekezaji.
Wanapozungumza wakazi hao wanasema ya kuwa pesa walizolipwa zilikuwa chini ya kiwango. Kuna mama mmoja alisikika akisema alilipwa
shilingi milioni 27, na hajapewa kiwanja. Maana yake ni kwamba katika hiyo milioni 27 anunue kiwanja na ajenge nyumba ya kuishi yeye na familia yake. Halafu wiki iliyopita wakapewa siku saba wawe wamehama, wakati huenda hata hiyo milioni 27 wameshaitumia hata kama si yote kwa matumizi mengine. Kweli kama sio kuwapa watu ufukara wa kudumu ni nini? 

No comments: