![]() |
| Prof,Kitila Mkumbo. |
Pia
Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya
kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu..
Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang’anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.
Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo. “Hivyo Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.” Aliongeza: “Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.” Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku CCM ikiwa na viti 188. “Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,”alisema Profesa Mkumbo na kuongeza; “...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano. Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi. Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.”

No comments:
Post a Comment