![]() |
| Mh,Rais J.M.Kikwete. |
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Serikali imesema kuwa siku ya kesho ni mapumziko, Ombeni Sefue ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi,na Mwenyekiti wa kamati ya kuingiza serikali mpya madarakani,kwa niaba ya serikali amesema kuwa kesho ni siku ya mapumziko kwa sababu rais anayo mamlaka ya kutangaza siku yoyote kuwa ni mapumziko kwahiyo rais ameamua kuwa kesho iwe ni siku ya mapumziko ili wananchi waweze kusheherekea kuhitimishwa kwa awamu ya nne kuingia awamu ya tano kama kawaida tunatarajia wananchi waanze kuingia kuanzia saa kumi na mbili asubuhi kwenye uwanja wa Uhuru.
‘’Mambo muhimu yatakayokuwepo ni gwaride na magwaride hayo yapo mawili kuna gwaride la kumuaga rais anayeondoka halafu kuna gwaride la kumkaribisha rais mteule na makamu wa rais mteule na kuapishwa na jaji mkuu’’Alisema Ombeni Sefue.

No comments:
Post a Comment