Wednesday, 4 November 2015

WANANCHI WILAYANI MVOMERO-MOROGORO WASHIRIKI MAJI YA KUNYWA NA MIFUGO.

Wananchi wa kijiji cha wami Sokoine wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wamelalamikia kutumia maji machafu yanayotumiwa na mifugo kwa muda mrefu hali inayotishia afya za wananchi hao kwa kuhofia kupata magonjwa. Wakizungumza kwa masikitiko wananchi hao wamesema wanalazimika kununua maji shilingi 1,500 kila dumu la lita 20 ambapo wamesema wanashangazwa na hatua ya serikali kushindwa kufanya jitihada za kuwapatia maji wananchi wa kijiji hicho hali ya kuwa wanalipa kodi kama watanzania wa maeneo mengine.

No comments: