Kwa
Mara ya kwanza tangu akumbwe na 'sekeseke' la ziara ya kushtukiza na
Serikali katika kituo chake cha tiba mbadala, Tabibu J.J Mwaka
amezungumza na Times FM kufafanua tukio hilo.
Akizungumza kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM, Mwaka amesema Uwezo wake kitaaluma hauna shaka kwani amesomea nchini China na ndio maana Serikali imempa usajili kwa kutambua uwezo wake.
"Taaluma yangu haina mushkeri, ukizungumzia China ndio inaongoza kwa Tiba asili duniani, nimesoma kule na hili halina shaka" alisema.
"Nimesoma Nina taaluma, asiyetaka aje tupimane uwezo" ameongeza.
Akijibu swali lililoulizwa na Mtangazaji Mariam Kitosi kuhusiana na kuvunja sheria kwa kujiita DAKTARI, Tabibu huyo amedai haoni tatizo kuuitwa hivyo na hato acha kujiita Dr kwa kuwa ni katika matumizi tu ya Lugha.
"Ukisema Tabibu ni Kiarabu, ambapo kiswahili ni Mganga, na kingereza ni Dr. Tatizo likowapi?"
Akifafanua kuhusu kumkimbia Naibu Waziri wa Afya Dr Hamis Kigwangala, kwa kuruka ukuta ofisini kwake Fore Plan Clinic, Mwaka amesema ni walipishana tu kwa kuwa hakuwa na taarifa ya ujio wa Waziri huyo.
"Mchapakazi anamjua mchapakazi mwenzie, alipata feelings kama hizo (kukimbiwa), ukweli nilitoka kabla hajafika na sikuwa na taarifa kama angefika" Alisema.

No comments:
Post a Comment