Thursday, 14 January 2016

MAALIM SEIF AMWANDIKIA BARUA POPE FRANCIS KUHUSU SINTOFAHAMU INAYOENDELEA ZANZIBAR.

katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad
Katika harakati za kutafuta suluhu za mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar, mgombea kiti cha Urais visiwani humo na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad amemuandikia barua kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ili aingilie kati.
Taarifa ya CUF imedai kuandika barua hiyo Novemba mwaka jana, ikimuomba Papa kutumia nguvu yake aliyonayo kwa jamii ajaribu kuingilia kati sintofahamu inayoendelea.
Chama tawala CCM na chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF, vinavutana kisiasa huku CUF ikidai uamuzi wa CCM kutaka kurudiwa kwa uchaguzi ni kubaka demokrasia ya Wazanzibar.
Barua hiyo imetumwa tangu Novemba mwaka jana, huku chama hicho kikikiri kutopokea majibu ya barua hiyo mpaka leo.

No comments: