 |
Mbwana Samata akiwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akutana na waandishi wa habari
asubuhi ya leo katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ndogo ya CCM
Lumumba Jijiji Dar es salaam.
Mheshimiwa Kikwete ametembelewa ofisini kwake na mwanasoka bora Afrika
kwa wachezaji wa ndani Mbwana Samata asubuhi hii na kufanya nae
mazungumzo ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kwa mafanikio hayo makubwa
ambayo Mbwana ameyapata na heshima kubwa aliyoiletea Taifa kwa ujumla.
Baada ya mazungumzo hayo Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, Mbwana
Samata pamoja na Muenezi wa CCM ambaye pia ni Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye walikutana na waandishi wa
habari na kuzungumzia mafanikio ya Samata na Kama Chama wamepokea vipi
mafanikio hayo.
 |
Nape Nnauye akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Lumumba. |
 |
Waandishi wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Samata na Mhe Jakaya Kikwete | |
No comments:
Post a Comment