Serikali yakata Rufaa kupinga kuachiwa huru kwa Sheikh Ponda.

Uhuru
wa Sheikh Issa Ponda umeingia katika sura nyingine kufuatia uamuzi wa
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi
uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro, ulioumuachia
huru kiongozi huyo wa dini aliyekuwa anakabiriwa na mashataka ya
uchochezi.
Hatua hiyo imetangazwa jana na Mwanasheria mwandamizi wa Ofisi ya DPP,
Bernard Kongola, mwanasheria huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa
tayari upande wa mashtaka umeomba nakala ya hukumu na nyaraka za
mwenendo wa shauri hilo ili waweze kukata rufaa Mahakama Kuu.
Hata hivyo, alieleza kuwa bado upande wa mashtaka haujapewa nakala ya
hukumu hiyo ingawa wameanza kuiomba muda mrefu uliopita, kitu ambacho
amedai kinawashangaza.
“Hatujui kuna tatizo gani, maana tunapoomba kupatiwa nakala ya hukumu,
hakimu amekuwa anatuambia kwamba bado hawajamaliza kuichapa, kwa kweli
hii inashangaza,” Alisema.
Sheikh Ponda na wenzake waliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi
Morogoro, Novemba 30 mwaka jana baada ya kutowakuta na hatia katika
makosa ya uchochezi na kukiuka amri ya mahakama. Kesi ambayo ilianza
kusikilizwa tangu Mwaka 2013.
Chanzo: Dar 24
No comments:
Post a Comment