Thursday, 14 January 2016

SERIKALI{Tz}YAMZAWADIA SAMATA KIWANJA-KIGAMBONI.

Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi, amemkabidhi zawadi ya kiwanja kilichopo Kigamboni mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta kama njia ya kuthamini tuzo ya mchezaji bora wa Afrika aliyoipata.
Lukuvi amemkabidhi zawadi hiyo katika hafla iliyofanyika Hyatt Regency na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa.
Mbali na zawadi hiyo, Samatta amekabidhiwa fedha taslimu ambazo haijajulikana ni kiasi gani.
Mbwana Samatta aliyekuwa akicheza mpira wa kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayomilikiwa na tajiri wa madini  na aliyewahi kuwa Gavana wa jimbo la Katanga nchini humo Moise Katumbi anatarajiwa kujiunga na timu ya  KRC Genki ya Belgium barani ulaya,  Hafla hiyo imefanyika usiku huu jijini Dar es salaam.

No comments: