Thursday, 14 January 2016

TAARIFA ZA KUWASILI MWILI WA MAREHEMU LETICIA NYERERE.

Marehemu Leticia Nyerere
Kuna uwezekano mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Leticia Nyerere, aliyefia nchini Marekani utawasili nchini mapema kwa ajili ya maziko tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa awali.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Rose-Mary Nyerere, alisema Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi, kwa kushirikiana na familia hiyo wanafanya jitiahada kuusafrisha mwili huo kuja nchini kabla ya Jumatatu iliyokuwa imepangwa awali.
“Ratiba inaonyesha mwili utawasili nchini Januari 18 kulingana na taratibu za safari, ila tunajaribu kuangalia njia ya kufupisha muda huo kwa sababu ni mbali tangu mpendwa wetu Leticia alipotutoka,” aliasema.
Alisema mwili huo baada ya kuwasili nchini utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Msasani, jijini Dar es Salaam na taratibu za kuusafirisha kwenda kijijini Butiama, mkoani Mara kwa ajili ya maziko zitaendelea.

No comments: