Monday, 4 January 2016

TRA YAKAMATA SHEHENA YA MAFUTA YA OKI YALIYOTAKA KUTOROSHWA NJE YA NCHI,


Mamlaka ya mapato nchini TRA mkoani Morogoro imekamata madumu 1,599 ya mafuta ya kula aina ya OKI yaliyokua yakisafirishwa kwenda nje ya nchi bila kulipiwa ushuru.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake meneja wa TRA mkoa wa Morogoro Philip Kimune amesema wamekamata shehena hiyo ya mafuta baada ya kupitishwa nchini kwa njia za magendo na hayakuwa yamelipiwa kodi halali ya TRA ambayo ni shilingi milion 64.7 hivyo kuamua kuutaifisha mzigo huo.
Baada ya kukamatwa kwa mafuta hayo, TRA mkoa wa Morogoro wamewasiliana na ofisi ya kamishna wa forodha na kupewa jukumu la kuyagawa mafuta hayo kwa taasisi za serikali sambamba na vituo vya watoto yatima ambapo kwa upande wa magereza mkoa wa Morogoro wamepata madumu 804, hospitali ya mkoa wa Morogoro madumu 480 sambamba na vituo vingine vya watoto yatima ambavyo vitagawana madumu 105 kwa kila mmoja.
Wanufaika wa mgao huo waliofika mapema kuchukua mafuta hayo wametoa shukrani zao kwa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kuwakumbuka ambapo ASP Zephania Neligwa akizungumza kwa niaba ya gereza la mahabusu la mjini Morogoro amesema badokuna uhitaji mkubwa wa msaada kwa maeneo kama hayo.

No comments: