Thursday, 7 January 2016

WASANII{TZ} WAUPINGA UONGOZI WA COSOTA.

Wakali  wa muziki nchini wameukataa uongozi wa Cosota kwa madai kuwa una usimamizi mbaya wa kazi zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari,  walisema hawana imani na uongozi wa Cosota na kampuni ya kusimamia kazi za wasanii Afrika Mashariki (CMEA).
“Hatuna imani na Cosota, CMEA na Basata kutokana na kushindwa kusimamia kazi zetu. Hata mchakato uliotumika kupata viongozi wa mashirikisho hayo si sahihi kwa upande wetu kwa kuwa viongozi waliopo ndani ya uongozi huo hakuna hata mmoja ambaye ni msanii,” alisema Mwana FA.
Katika ‘line’ nyingine, umoja wa wasanii hao unatarajia kupeleka malalamiko yao kwa Waziri wa habari, utamaduni, wasanii na michezo Nape Nnauye.

No comments: