Thursday, 14 January 2016

Wastara Ampa Masharti Magumu zilipendwa Wake.

Bond Bin Suleiman
Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amempa wakati mgumu aliyekuwa mwandani wake ambaye pia ni meneja wake, Bond Bin Suleiman kuwa kama bado anataka waendelee kufanya kazi pamoja asiendekeze wivu baada ya yeye kuolewa.
Wastara na Mumewe aliyeolewa naye Juzi ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Khamis

Wastara aliyeolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Khamis alisema kuwa ni ukweli usiopinga kwamba yeye na Bond walikuwa wapenzi, kwa kuwa sasa ameolewa na mkataba wake na Bond bado haujaisha imempasa ampe masharti.
Wastara na Bondi

“Ninachotaka tuendelee kufanya kazi na azingatie kuniheshimu na kusahau kabisa kama tuliwahi kuwa wapenzi, pia muamuzi wa mwisho ni yeye kama ataona hawezi basi maana nimeshaandaa mtu mwingine,” alisema Wastara.

Chanzo: GPL

No comments: