Friday, 29 January 2016

WAZIRI MKUU ATOA MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU TBC KURUSHA MATANGAZO YA BUNGE LIVE.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa usitishwaji wa matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) utabaki palepale.“Msimamo wa TBC ni msimamo wa Serikali,” amesema Majaliwa jana wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kufahamu kauli ya serikali juu ya TBC kusitisha matangazo kwani ni haki ya wananchi kikatiba.
Waziri Mkuu alisema suala hilo lilishatolewa ufafanuzi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kilichofanywa na TBC ni kubadilisha ratiba. “Huo ni mpango wa ndani wa taasisi yenyewe kujiendesha, msimamo wa TBC ni msimamo wa serikali,” alieleza.

No comments: