![]() |
| Hali ya Mkongwe wa Muziki wa Takeu, Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’. |
Picha inayomuonesha Nice akiwa amepungua
mwili ilizagaa mapema wiki hii kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi
waliochangia mjadala wa picha hiyo, walisema staa huyo aliyetikisa kwa
utajiri enzi hizo, kwa sasa atakuwa anaumwa sana huku mjadala mkubwa
ukawa ni ya lini?
![]() |
| Mr. Nice akiwa katika pozi, enzi zileee. |
Baada ya Ijumaa kuinasa
picha hiyo, lilifanya jitihada za kumpata msanii huyo kwa kumvutia waya
alipopatikana, alifunguka kwa kirefu kuhusu afya yake:
“Kwanza hiyo picha ni ya kitambo sana.
Si unakumbua lile sakata langu la mimi kulishwa sumu kwenye chakula?
Basi ndiyo kipindi kile.
“Namshukuru Mungu niliiwahi ile sumu na
kupewa dawa ambazo natumia mpaka sasa. Kweli nilipungua lakini ni wakati
huo, kwa sasa sipo hivyo kama kwenye hiyo picha inayosambazwa
mitandaoni,” alisema Mr. Nice.
Akaongeza kuwa ni kweli afya yake haiko
poa sana kwa kuwa bado anaendelea kutumia dawa za kuimaliza sumu ile
lakini siyo kama vile anavyoonekana kwenye picha hiyo (iliyopo ukurasa
wa mbele kushoto).
Chanzo-GPL


No comments:
Post a Comment