Tuesday, 5 April 2016

GADNER G HABASH ARUDI CLOUDS MEDIA.

Mtangazaji mkongwe nchini, Gadner G Habash, amerejea tena kwenye kituo chake cha awali, Clouds FM.
Gadner anajiunga tena na redio hiyo akitokea EFM alikokuwa akifanya kipindi cha jioni cha Ubaoni. Kabla ya EFM, Gadner alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha Times FM. Mtangazaji huyo anatarajiwa kurejea kwenye kipindi chake cha jioni, Jahazi.

Kwenye Interview yake na MKASI TV October 2014, Gardner G. Habash alisemanimeifanyia mambo mazuri bongofleva na ningependa kutumwa zaidi kufanya mambo mazuri, kingine kizuri zaidi kwenye show zangu napiga sana nyimbo za bongofleva kuliko nyimbo za kutoka sehemu nyingine’
Mtangazaji huyo anayejulikana kwa jina la utani ‘Captain’, anaingia kwenye kikosi cha Clouds FM ambacho hivi karibuni kilipata pigo baada ya watangazaji wake wawili, Gerald Hando na Paul James kuacha kazi. Wawili hao wanadaiwa kujiunga na EFM hivi karibuni.

No comments: