![]() |
| Gadner G Habash. |
Mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash amesema miongoni mwa vitu anavyojutia katika maisha yake ni kuachana na mke wa kwanza aliyezaa naye mtoto wa kike, Karen, ambaye kwa sasa yupo mwaka wa pili chuoni. Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gardner alisema kutokana na kubadilisha kazi ya awali na kuwa mfanyabiashara kipindi anaishi Mwanza, alijikuta akiiweka kwenye mawe ndoa yake kwa kukosa muda nayo. “Yale mazingira niliyokutana nayo Mwanza ya kibiashara yalisababisha nikaachana na mke wangu wa kwanza, ni kitu ambacho najuta,”alisema staa huyo. “Nisije nikasema sana mwisho nikalia hapa bure,” alisisitiza.
![]() |
| Karen |
Alidai kuwa yeye na Lady Jaydee hawana mawasiliano ya aina yoyote kwa sasa na mara ya mwisho walikutana kipindi wanakamilisha taratibu za talaka. Kwa upande mwingine Gardner amedai kuwa maisha aliyonayo sasa ni ya furaha tele. Mtangazaji huyo amejiunga tena na Clouds FM akitokea EFM.


No comments:
Post a Comment