Friday, 1 April 2016

USO KWA USO MAHAKAMANI KATI YA WAKILI WA Mh,JAMES MBATIA NA AUGUSTINO LYATONGA MREMA KWENYE KESI YA UCHAGUZI-{2015}.

Mwenyekiti taifa wa chama cha TLP, Agustin Mrema, amefungua kesi ya kupinga matokeo iliyompa ushindi mwenyekiti wa NCCR, James Mbatia.
Kesi hiyo imeendelea kushuhudiwa huku kukitokea sintofahamu katika majibu ya Mrema, baada ya kukanusha kukamata vipeperushi vya kumchafua mitaani.
Tazama hapo chini majibizano kati ya wakili wa Mbatia na Mzee Mrema,
Wakili: Hivi Mzee Mrema, ulikuwa ukihudhuria mikutano ya James Mbatia?
Shahidi: Hapana, nilikuwa natuma watu wangu wahudhurie na waniletee ripoti.
Wakili: Mzee Mrema, wewe ulikamata vipeperushi vingapi?
Shahidi: Mimi sikuhusika kukamata, nililetewa.
Wakili: Vipeperushi vilivyokamatwa Kilema Kati, uliletewa lini?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Kilema Kusini?
Shahidi: Tarehe 19, mwezi wa 10.
Wakili: Njia Panda?
Shahidi: Tarehe 19, mwezi wa 10.
Wakili: Kahe?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Kochakindo?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Marangu Makomu?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Rawia?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Mshihiri?
Shahidi: Tarehe 23, mwezi wa 10.
Wakili: Vipeperushi vya mwisho uliletewa lini?
Shahidi: Tarehe 25, siku ya kupiga kura.
Wakili: Hiyo tarehe 25, uliletewa vipeperushi vingapi?
Shahidi: Vilikuwa vingi, sikumbuki.
Wakili: Katika madai yako, ulisema makanisa yote yalisambazwa vipeperushi, mbona hukutaja kanisa la Uwomboni unakosali?
Shahidi: Sikukumbuka.
Wakili: Mzee Mrema, daktari wa uchumi na siasa, hebu tueleze katika vile vipeperushi 75 unavyodai uliletewa na kisha ukavikabidhi kwa msimamizi wa uchaguzi vipeperushi 74, kile kipeperushi kimoja ulichobaki nacho ulikifanyia nini?
Shahidi: Nilikitumia kuwaonyesha wananchi wangu kwamba kuna kipeperushi kinasambazwa kuonyesha kuwa mimi nimeridhia Mbatia agombee ubunge.
Wakili: Katika ugomvi wako na Mbatia, nini hasa kilikuudhi?
Shahidi: Nilisema logo yangu ni jogoo, halafu mimi sina kipara kama cha Mbatia, na pili kukosekana baraghashia yangu (kofia), na tatu matumizi mabaya ya picha yangu, tena bila ridhaa yangu.
Wakili: Kwani ulipeleka picha yako Tume ya Uchaguzi?
Shahidi: Ndiyo, nilipeleka kwa ajili ya uchaguzi.
Wakili: Una miaka mingapi sasa hivi, Dk. Mrema?
Shahidi: Miaka 72.
Wakili: Jimbo la Vunjo lilikuwa na vituo vingapi vya kupigia kura?
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili: Uliweka mawakala vituo vyote?
Shahidi: Ndio, niliweka vituo vyote.
Wakili:Kwani mawakala wako walikusaliti?
Shahidi: Baadhi yao, walinisaliti.
Wakili: Mwaka 2014, ulikuwa Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, na ulishiriki uchaguzi wa serikali za mitaa. Kweli, si kweli?
Shahidi: Kweli.
Wakili Tibanyendera: Je, wakati huo wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vipeperushi vya James Mbatia vilisambazwa?
Shahidi: Hapana.
Wakili: Mzee Mrema, katika uchaguzi huo ulipata viti vinane tu kwenye vijiji. Kweli, si kweli?
Shahidi: Kweli.
Wakili: Unakumbuka NCCR-Mageuzi walipata vijiji vingapi?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: CCM walipata vingapi?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Chadema vingapi?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Kwa hiyo TLP ilianza kuanguka tangu mwaka 2014, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Kweli, si kweli?
Shahidi:  Ndiyo.
Wakili Tibanyendera: Kwa hiyo chama kilishaanza kupoteza uaminifu kwa wapigakura?
Shahidi: Si kweli.
Wakili: Jimbo la Vunjo unafahamu lina shule ngapi za msingi?
Shahidi: Sijui.
Wakili: Nakusaiidia, Vunjo ina shule za msingi zaidi ya 100. Sawa?
Shahidi: Inawezekana.
Wakili: Kuna taarifa katika hizo shule 100, miundo mbinu yake ya vyoo ni mibaya. Kweli, si kweli?
Shahidi: Kweli.
Wakili: Huoni kwamba shule hizo kukosa miundombinu bora ya vyoo, ndiko kumewafanya wananchi wakuhukumu na kukosa ubunge?
Shahidi: Hapana.

No comments: