Thursday, 2 June 2016

Mwaka 2015 ulikuwa sadaka kwangu -Abydad

Mtayarishaji wa muziki Abydad

Mtarishaji wa muziki ambaye kwa mwaka jana aliweza kutengeneza ngoma nyingi kali ikiwepo Namgharamia ya Christian Bella na Alikiba, Chekecha ya Alikiba, Subira ya Kassim Mganga  na zingine nyingi amefunguka na kusema kuwa mwaka 2015 kwake ilikuwa mwaka wa sadaka.
Abydad akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS amesema kuwa aliutumia mwaka huo kufanya kazi na wasanii wakubwa ili kwanza kujitangaza vyema na kuweza kujitambulisha kwa watanzania na kudai kuwa mwaka huo amefanya kazi kwa hasara hasara sana. "Kitu cha kwanza mwaka jana nilipanga kujitambulisha kwenye muziki vizuri nilipanga nijulikane, hivyo ili utambulike ilikuwa ni lazima nitafute wasanii wakubwa ili nifanye nao kazi nashukuru hilo nilifanikiwa. Hivyo nilifanya kazi na wasanii wakubwa lakini kihasara hasara ili niweze kufikia malengo, lakini kwa sasa nafanya kazi na mwaka 2016 nimeanza na kazi mpya ya Alikiba 'Aje' zinakuja zingine kali sana naweza kusema kuwa sasa kazi imeanza 2016" alisema Abydad
Napenda kuwaambia tu mashabiki wa kazi zangu kuwa 2016 kuna mambo moto moto, mazuri na matamu nitaleta sound nyingine kwenye muziki wa bongo fleva kama ambavyo nimeanza na ngoma ya 'Aje' hivyo kuna zingine nyingi zinakuja" aliongezea Abydad

No comments: