Saturday, 21 April 2018

Masogange Afariki Dunia


Video queen maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia Aprili 20, 2018 katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada kuzidiwa ghafla jana na kukimbizwa hospitalini hapo
Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinadai Masogange alifikishwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na homa ya matumbo na tatizo la kupungukiwa na damu. Global Publishers imefika hospitalini hapo na kujionea umati wa watu waliokusanyika wakilia kwa uchungu kumpoteza msanii huyo.
Dkt. Kihama Ngoma ameithibitishia Global Publishers na kusema taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Tayari mwili wa marehemu Masogange umehaimshwa hospitalini hapo na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa.

No comments: