Monday, 3 June 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR WAAGWA RASMI LEO NCHINI AFRICA YA KUSINI.

MWAKILISHI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRICA YA KUSINI AKITOA NASAHA ZAKE MARA BAADA YA MWILI WA MAREHEMU KUAGWA RASMI NCHINI AFRICA YA KUSINI.
MWAKILISHI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRICA YA KUSINI,KINJEKETILE MWIRU NA MWAMVITA MAKAMBA WAKIWA NJE YA KANISA MWILI WA NGWAIR ULIPOAGWA NCHINI AFRICA YA KUSINI.
KANISA AMBAPO MWILI WA ALBERT MANGWAIR ULIAGWA NCHINI AFRICA YA KUSINI LEO.
WATANZANIA WAISHIO NCHINI AFRICA YA KUSINI WAKIUAGA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR LEO JIONI NCHINI AFRICA YA KUSINI.
JENEZA LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR.
MWILI WA ALIYEKUWA MSANII WA MUZIKI WAKIZAZI KIPYA NCHINI MAREHEMU ALBERT MANGWAIR a.k.a NGWAIR{COWBAMMA}UMEAGWA RASMI LEO JIONI NCHINI AFRICA KUSINI,KWA MUJIBU WA RATIBA ILIYOTOLEWA NA KAMATI YA MAZISHI YA MSANII HUYO NCHINI,KILICHOKUWA KINASUBIRIWA NI TARATIBU KUKAMILIKA JUU YA KUUSAFIRISHA MWILI WA MSANII NGWAIR TOKA NCHINI AFRICA YA KUSINI,TARATIBU AMBAZO ZIMESHAKAMILIKA KWA ASILIMIA 90% NA KINACHOFUATA NI KUWASILI KWA MWILI WA MSANII HUYO MAHIRI NCHINI KESHO MAJIRA YA SAA NANE MCHANA,TAHARIFA YA KAMATI IKISOMWA NA MSEMAJI WA KAMATI BW, ADAM JUMA INAWATAKA WAPENZI WOTE WA MANGWAIR,WAPENZI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA KUJITOKEZA KWA WINGI UWANJA WA NDEGE WA TAIFA{DAR ES SALAAM-TERMINAL ONE}KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU KWA PAMOJA,TAYARI KWA KUAGA SIKU YA J/TANO VIWANJA VYA LEADERS CLUB KINONDONI JIJINI NA HATIMAYE KUSAFIRISHWA HADI MKOANI MOROGORO ALIKO MAMA YAKE KWA AJILI YA MAZISHI.

MTOTO WA MWANASIASA MAARUFU NCHINI MZEE MAKAMBA,MWAMVITA MAKAMBA AKIUAGA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR LEO NCHINI AFRICA YA KUSINI.
RUTA BUSHOKE MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA ALIYEKO NCHINI AFRICA YA KUSINI KWA SASA NI MMOJA KATI YA WATU WALIOONYESHA USHIRIKIANO MKUBWA KUKAMILISHA KULETWA KWA MWILI WA MAREHEMU NGWAIR NCHINI,
MWENYE FULANA NYEUSI NI MMOJA KATI YA RAIA WA TANZANIA WAISHIO NCHINI AFRICA KUSINI.AKIWA PAMOJA NA KINJEKETILE MWIRU KATIKATI MUDA MFUPI BAADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU NGWAIR.

ANGALIA VIDEO JINSI WATANZANIA WALIVYOUAGA MWILI WA ALBERT MANGWAIR NCHINI AFRICA YA KUSINI:-

No comments: